Wito umetolewa kwa wakenya kuwa mstari wa mbele kuwasamehe waliowakosea kudhirisha upendo wao na kuunganika kwa manufaa ya kuishi wa amani.
Akiongea katika kanisa la Holy Family Minor wakati wa misa ya jumatano ya majivu askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nairobi Philip Anyolo amesema kwamba wakenya wanastahili kuweka kando tofauti zao na kuhakikisha wamewasamehe wengine ikiwa ni ishara tosha ya undugu mwema.
Vilevile askofu Anyolo amewataka wakenya kuwa na huruma kwa wale ambao hawana uwezo wa kupata chakula ama wanapitia changamoto si haba katika maisha akiwahimiza kuwa wakenya wanaopendana.
Kauli hii ikiungwa mkono na askofu mkuu wa jimbo kuu katoliki la Nyeri Anthony Muheria ambaye amewataka wananchi kuwasaidia wenzao wanaokabiliana na baa la njaa kutokana na ukame ambao umekithiri kwa muda sasa akiwaeleza kwamba msimu wa kwaresma ni kujali wasiokuwa na lolote katika jamii na kuwa karibu nao maishani.
Maaskofu hao wameongea wakati na ambapo kanisa katoliki ilianza rasmi mfungo wa siku arobaini ya kwaresma kilele chake kikiwa pasaka ,kauli kuu mwaka huu kutoka kwa muungano wa maaskofu wa kikatoliki nchini KCCB ikiwa upatanisho.